Rais William Ruto ametuma risala za rambi rambi kwa familia, jamaa, marafiki na raia wa Zambia kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Edgar Lungu.
“Tunatuma rambirambi kwa familia na wananchi wa Zambia, kufuatia kifo cha ghafla cha Edgar Lungu,” alisema Rais Ruto kupitia ukurasa wa X.
Alimtaja Lungu kuwa kiongozi shupavu aliyewahudumia wananchi wa Zambia kwa kujitolea.
“Mungu awape raia wa Zambia nguvu na faraja wakati huu mgumu,” aliongeza Rais Ruto.
Lungu alifariki alipokuwa akipokea matibabu katika kituo kimoja cha Afya Jijini Pretoria, Afrika Kusini, kulingana na chama chake cha Patriotic Front.
Aliongoza Zambia kwa miaka sita kuanzia 2015, na kushindwa katika uchaguzi na Rais wa sasa na Hakainde Hichilema kwa kura nyingi.