Rais Ruto amwomboleza mwenyekiti wa KNCHR

Mwenyekiti huyo wa KNCHR Roseline Odede aliripotiwa kufariki Ijumaa Januari 3, 2025, baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Marion Bosire
1 Min Read

Rais William Ruto ameongoza viongozi wengine katika kumwomboleza mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya kutetea haki za binadamu KNCHR, Roseline Odede aliyefariki Ijumaa baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Katika taarifa iliyochapishwa kwenye kitandazi cha X, Rais alisema amehuzunishwa na kifo cha Odede huku akimtaja kuwa mpiganiaji shupavu wa haki za binadamu na mtetezi wa jamii yenye usawa.

Naibu Rais Kithure Kindiki alimtaja marehemu Odede kuwa mtaalamu wa sheria aliyejitolea kwa kina kupigania haki na uhuru wa binadamu.

Aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga naye amemwomboleza Odede kama wakili aliyekamilika, aliyeafikia ufanisi katika kulinda haki za binadamu na mfanyakazi wa umma aliyeheshimika sana.

Rais wa chama cha wanasheria nchini LSK Faith Odhiambo, amemtaja Odede kuwa mtu aliyekuwa na uelewa wa hali ya juu, aliyewapa nafasi wote na mshirika mwema ambaye alitoa kipaumbele kwa huduma kwa watu.

Odhiambo alisema kifo cha Odede ni hasara kubwa kwa taifa na kwa jamii nzima ya watetezi wa haki za binadamu.

Katibu wa usalama wa taifa na utawala wa kitaifa Raymond Omollo anasema kujitolea kwa Odede kuhakikisha haki na haki za binadamu zinadumishwa kunaacha urithi wa ufanisi na msukumo.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *