Rais Ruto ampongeza Donald Trump

Tom Mathinji
1 Min Read
Donald Trump ashinda uchaguzi wa Marekani 2024.

Rais William Ruto amempongeza Donald Trump kufuatia kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa 47 wa Marekani.

Katika ujumbe wa pongezi kwenye mtandao wa X, Rais Ruto alitaja ushindi wa Trump kuwa ishara raia wa Marekani walitambua uongozi wake ulio na maono, ujasiri na wenye uvumbuzi.

Ruto alidokeza kuwa Kenya iko tayari kuimarisha ushirkiano wake na Marekani katika biashara, uwekezaji, teknolojia, amani na maendeleo endelevu.

Kiongozi huyo wa taifa pia alielezea matumaini kwamba uongozi wa Trump utatoa fursa ya kushirikiana na Kenya katika kushughulikia changamoto zinazokabili dunia na kuharakisha maendeleo ya kiuchumi.

“Tunatazamia kukuza ushirikiano chini ya uongozi wako tunaposhirikiana katika kutatua changamoto za dunia, kudumisha amani na usalama na kuimarisha ukuaji wa uchumi kwa manufaa ya watu wetu,” alisema Rais Ruto.

Share This Article