Rais William Ruto amefanya mazungumzo na mwenzake wa Botswana Gideon Boko mapema leo Jumatano jijini Accra, Ghana.
Wakati wa mkutano kati yao, wawili hao walijadiliana kuhusu masuala kadhaa ikiwemo ushirikiano kati ya Soko la Pamoja la Mataifa ya Mashariki na Kusini mwa Afrika (COMESA), Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki, (EAC).
Viongozi hao aidha walijadiliana jinsi COMESA, EAC na SADC zinaweza kubuni soko la pamoja la watu milioni 700 ili kupanua uwezo wa Afrika na kuondoa umaskini.
Ruto pia alimpigia debe Raila Odinga anayegombea wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC.
Boko amekubali kumuunga mkono Raila katika azima yake.