Rais Ruto akosa kutia saini mswada wa fedha wa mwaka 2024

Marion Bosire
1 Min Read
Rais William Ruto.

Rais William Ruto ametangaza kwamba hatatia saini mswada wa fedha wa mwaka 2024 ulioghubika na utata na anaurejesha sasa katika bunge la taifa.

Hatua hii inafuatia maandamano ya kupinga mswada huo yaliyotekelezwa jana na kizazi cha Gen Z ambapo waandamanaji walifika katika majengo ya bunge punde baada ya mswada huo kupitishwa humo.

Akizungumza katika ikulu ya Nairobi, Rais ambaye alikuwa na wabunge na magavana wa mrengo tawala wa Kenya kwanza amesema kwamba ameshauri wangunge wa mrengo huo kutupilia mbali mswada huo.

Alisema kwamba amesikiliza vilio vya wakenya ambao wamekuwa wakipaaza sauti kuupinga ndiposa ameamua kutoutia saini na kuurejesha bungeni ili uondolewe.

Kiongozi wa nchi aliwashukuru wabunge waliounga mkono mswada huo bungeni jana.

Rais Ruto alipendekeza mjadala wa kitaifa kuhusu jinsi ya kusimamia mipango ya nchi na jinsi ya kushughulikia nakisi ya bajeti.

Alisema pia kwamba ataandaa mkutano na vijana wa taifa hili almaarufu Gen Z ili kufahamu yanayowasibu na mapendekezo yao.

 

 

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *