Rais Ruto ahakikishia Wakenya kujitolea kwa serikali kuboresha maisha yao

Rais Ruto alisisitiza kwamba serikali yake imeweka mikakati ambayo itabadilisha nchi hii na kuhakikisha urejesho kamili wa kiuchumi.

Marion Bosire
1 Min Read

Rais William Ruto kwa mara nyingine amehakikishia Wakenya kujitolea kwa serikali kuboresha maisha yao.

Akizungumza alipohudhuria ibada leo Jumapili katika kanisa la Soul Harvest, kaunti ya Taita Taveta, kiongozi wa nchi alitaja kupungua kwa bei ya bidhaa za msingi.

Kulingana naye, uchumi wa taifa unaboreka hatua kwa hatua huku bei ya mafuta ikipungua pakubwa.

Rais Ruto alisisitiza kwamba serikali yake imeweka mikakati ambayo itabadilisha nchi hii na kuhakikisha urejesho kamili wa kiuchumi.

Kuhusu ajira, Rais alisema kwamba serikali inajitahidi kutengeneza fursa za ajira kwa vijana kupitia mpango wa kuwatafutia ajira nje ya nchi, mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu na vituo vya kidijitali.

Alisema serikali inatumia teknolojia na uvumbuzi kutoa nafasi za ajira na kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira humu nchini.

Aliwataka Wakenya wawe makini na wajiepushe na habari potovu zinazolenga kuhujumu maendeleo, kudunisha demokrasia na kuyumbisha taifa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *