Rais William Ruto leo amefanya ziara ya kikazi katika kaunti za Laikipia na Nyandarua. Alianzia katika kaunti ndogo ya Laikipia Mashariki ambapo aliweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu.
Mradi huo wa Nanyuki ni wa nyumba zipatazo 200 na kulingana na kiongozi wa nchi, watu zaidi ya 1000 watajipatia kipato kutokana na mradi huo.
Alitetea miradi hiyo ya nyumba akisema kwamba ni njia inayoelekeza wakenya kwa maisha mazuri ya baadaye ambapo familia zitapata fursa ya kumiliki nyumba.
Rais Ruto alianzisha pia mradi wa kuweka lami barabara ya Lamuria-Solio-shule ya msingi ya Kihara katika kaunti hiyo ya Laikipia.
Baadaye alitua katika kaunti ya Nyandarua ambapo alizindua kiwanda cha kutayarisha maziwa cha KCC.