Rais Ruto abashiri kwamba Kenya itakuwa taifa lililostawi

Marion Bosire
1 Min Read

Rais William Ruto amebashiri kwamba Kenya itabadilika kutoka kuwa taifa linalostawi hadi taifa lililostawi katika muda wa miaka 30 ijayo.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 70 ya uwepo wa kanisa la African Inland, Ziwani, kaunti ya Nairobi jana, Rais Ruto alisema kwamba utawala wake umeweka msingi wa kuafikia hadhi hiyo mwaka 2055.

Rais alisema ameshauriana na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, kiongozi wa ODM Raila Odinga na mwenyekiti wa KANU Gideon Moi aliyejiunga na serikali jumuishi hivi maajuzi kuhusu maono hayo.

Alisisitiza kwamba serikali ina maono halisi na mpango wa kubadili uchumi na kuimarisha hali ya maisha ya wananchi wote kote nchini.

Katika hotuba yake, Rais Ruto alitangaza pia ushirikiano kati ya serikali ya kitaifa na serikali ya kaunti ya Nairobi kwa lengo la kutatua tatizo sugu la taka na ukosefu wa taa za barabarani hali inayochangia ongezeko la uhalifu.

Website |  + posts
Share This Article