Rais Ramaphosa atetea uwekezaji wa Marekani barani Afrika hasa sekta ya madini

Marion Bosire
1 Min Read

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema kwamba uwekezaji wa Marekani barani Afrika unaweza kusaidia nchi za Afrika kufaidika sana na madini yake muhimu na kukuza uchumi wake kwa kustawisha sekta ya viwanda.

Alikuwa akizungumza kwenye ufunguzi wa kongamano muhimu la kibiashara kati ya Marekani na Afrika jijini Johannesburg,ambapo alisema Afrika ni kitovu cha malighafi muhimu, lakini waafrika hawataki kufahamika tu kama wazalishaji wa bidhaa.

Ramaphosa aliongeza kusema kwamba nchi za Afrika zitafaidi pakubwa kwa kusalia na malighafi hizo na kuzibadilisha kuwa bidhaa ambazo zinaweza kuuzwa ulimwenguni, kuliko kuuza nje malighafi kwa nchi ambazo zina uwezo mkubwa wa kiviwanda.

Africa ina asilimia 40 ya dhahabu yote ulimwenguni kulingana na umoja wa mataifa na ina madini mengi ya cobalt, uranium, platinum na diamond.

Kongamano hilo la Johannesburg linaangazia sera ya hali ya ukuaji wa Afrika siku za usoni na fursa, mpango wa kibiashara uliopitishwa mwaka 2000, ili kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Marekani na Afrika.

Website |  + posts
Share This Article