Rais Raisi wa Iran sasa kuwasili nchini Jumatano

Martin Mwanje
1 Min Read
Rais wa Iran Ebrahim Raisi sasa atawasili humu nchini kesho Jumatano kwa ziara ya kitaifa. 
Rais Raisi alikuwa amepangiwa kuwasili nchini leo Jumanne.
“Ziara hiyo ilipaswa kutoa nafasi kwa nchi hizo mbili kufanya mapitio na kuuhuisha uhusiano wa pande mbili kwa manufaa ya raia wa nchi hizo,” ilisema Wizara ya Mambo ya Nje katika taarifa.
“Ratiba ya Rais sasa imepitiwa upya ili kuruhusu kumaliziwa kwa Makubaliano makuu ya Maelewano ambayo ni muhimu katika kuboresha uhusiano zaidi. Rais wa Iran sasa atawasili nchini kesho kwa ziara ya kitaifa.”
Punde atakapowasili, Rais Raisi ataelekea Ikulu ya Nairobi kwa mkutano wa pande mbili utakaoanza saa moja asubuhi.
Kisha ataenda kuweka maua kwa kaburi la hayati Mzee Jomo Kenyatta kabla ya kuzuru nchi zingine za Afrika.
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *