Rais Museveni amsifu mchungaji Dorcas Rigathi

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemmiminia sifa sufufu  mkewe naibu Rais wa Kenya mchungaji Dorcas Rigathi, akimtaja kiongozi wa kupigiwa mfano aliyejitolea vilivyo katika kazi yake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kitabu Jesus’Africa, kilichoandikwa na Bintiye Rais wa Uganda  Patience Museveni Rwa-Bwogo, katika Ikulu ya Rais mjini Entebbe Museveni alimpongeza mchungaji  Dorcas Rigathi kwa kueneza Injili.

“Tulipokuwa tukiapisha serikali mpya, nilikuwepo lakini mchungaji Dorcas hakuzumgumza, lakini nimeshangaa kuona mtu shupavu hapa, nitajifunza mengi kutokana na ujuzi wake wa uchungaji,” alisema Rais Museveni.

Mchungaji Dorcas aliyekuwa msemaji rasmi wakati wa hafla hiyo alimpongeza Rais Museveni kwa kuwa kiongozi mwenye msimamo thabiti sio tu Barani Afrika bali duniani kote.

Aidha, mchungaji Dorcas alitoa wito kwa raia wa Afrika kulinda familia zao dhidi ya vishawishi na vitisho vya mienendo isiyofaa duniani.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *