Rais mstaafu wa Kenya Uhuru Kenyatta amezuru mjini Abidjan, Ivory coast kuhudhuria kikao cha 15 cha kueneza amani, usalama na uthabiti barani Afrika.
Uhuru anaongoza ujumbe wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, EAC na ni miongoni mwa wajumbe wa Afrika wa Umoja wa Afrika, AU.
Kikao hicho kitaandaliwa kati ya Oktoba 25 na 26 mjini Abidjan, Côte d’Ivoire.
Miongoni mwa maswala yatakayojadiliwa ni mikakati ya AU, iliyopo na inayostahili kudumisha amani na mbinu za kukabiliana na mizozo barani Afrika.