Rais mstaafu Uhuru Kenyatta atoa wito wa umoja nchini

Tom Mathinji
1 Min Read

Rais mstaafu Uhuru Kenyatta, ametoa wito kwa viongozi wa taifa hili kupigia debe umoja wa Kitaifa na kupiga kumbo siasa za ukabila ambazo zinawagawanya wakenya.

Akizungumza Leo wakati wa kutawazwa kwa Askofu mteule Peter Kimani Ndung’u kuwa Askofu wa kabisa katoliki dayosisi ya Embu,, Uhuru alisema taifa hili linaweza tu piga hatua iwapo viongozi wataungana pamonja.

“Tuombee nchi yetu. Tuombee amani na uwiano kati ya viongozi na wananchi. Tuwache mambo ya ukabila na tupendane. Sisi wote ni Wakenya,” alisema Rais huyo mstaafu.

Aidha aliwahimiza viongozi kushughulikia mahitaji ya wakenya, badala ya kujihusisha kwa siasa za migawanyiko.

“Kenya haiwezi kufaulu watu wakiwa wametengana, kutupiana maneno na kukoseana heshima. Viongozi mheshimu wananchi na watarudisha hiyo heshima,”stated Uhuru

Akiwa Rais mstaafu, Uhuru alidokeza kuwa amekuwa akifuatilia kwa karibu matukio ya hapa nchini, lakini akaelezea matumaini kuwa taifa hili litasalia katika mkondo ufaao.

“Siku hizi mimi sina story mingi. Mimi naangalianga tu TV na kuskia redio tu,” he said

Share This Article