Rais wa Gabon Ali Bongo amestaafishwa, mkuu wa walinzi wa rais wa nchi hiyo ameliambia gazeti la Ufaransa la Le Monde.
“Yeye ni mkuu wa nchi ya Gabon. Amestaafu na anafurahia haki zake zote. Yeye ni raia wa Gabon wa kawaida, kama mtu mwingine yeyote,” Jenerali Brice Oligui Nguema anasema.
Hapo awali ilionekana kuwa Nguema alikuwa amependekezwa na viongozi wa mapinduzi kuchukua nafasi ya Ali Bongo, rais aliyeondolewa madarakani.
Kanda zilizopeperusha hewani hapo awali kwenye runinga ya serikali, zilimuonyesha akiinuliwa juu na wanajeshi wakiimba jina lake.
Lakini amekanusha uteuzi wowote kama huo.
“Sijitangazi, sifikirii chochote kwa sasa,” aliambia gazeti la Ufaransa.
“Ni mjadala tutakaofanya na majenerali wote.”