Kinara wa muungano wa Azimio Raila Odinga amekosoa mswada wa kifedha wa mwaka 2024/25, akisema lazima ufanyiwe marekebisho.
Kwenye taarifa, Odinga alisema mswada huo unakiuka matumaini ya wakenya waliotarajia kwamba serikali itapunguza mzingo wa ushuru.
Raila alisema mzigo wa sasa wa ushuru ndio wa wajuu zaidi tangu taifa hili lijipatie uhuru, huku huduma za umma zikiwa bado hazijaimarika.
Aliongeza kwamba mapendekezo ya kutoza ushuru bidha za kimsingi utaathiri pakubwa wakenya.
Raila alisema ushuru unaopendekezwa kutozwa bidha kama vile mkate,mafuta ya kupika,huduma za kifedha kupitia rununu na miwa utaathiri wengi.
Kinara huyo wa Azimio pia alikosoa ushuru wa asili mia 2.5 unaopendekezwa kutozwa wenye magari, bidha zinazotengezwa nchini pamoja na huduma za bima.
Alionya kuwa endapo mswada huo utapitishwa jinsi ulivyo,basi hatua hiyo itatikisa zaidi uchumi wa taifa hili.