Kiongozi wa mungano wa Azimio ,Raila Odinga anazuru eneo la Nyanza kati ya Ijumaa na Jumapili ,siku moja tu baada ya kuwatimu wabunge waasi katika chama cha ODM.
Odinga atafanya kikao na wajumbe wa ODM katika kaunti ya Migori siku ya Ijumaa kabla ya kuelekea kaunti jirani ya Kisii ambapo atafanya kikako eneo la Bomachoge Borabu kuhudhuria ibada siku ya Jumapili.
Yamkini Odinga aliwanusuru wabunge Mark Nyamita wa Uriri na Paul Abuor wa Rongo dhidi ya kutimuliwa badala yake wakatakiwa kuomba msamaha na kulipa faini ya shilingi milioni moja kila mmoja.
Katika kaunti ya Kisumu Raila Odinga tayari amewatimua waakilishi wadi wateule wanne waasi ambalo ni washirika wa karibu wa muungano wa Kenya Kwanza.