Waziri mkuu wa zamani Raila Odinga atahudhuria kongamano la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC litakaloandaliwa jijini Beijing kati ya Septemba 4 na 6, 2024.
Mataifa yote ya bara Afrika yatawakilishwa kwenye kongamano hilo isipokuwa Eswatini na tayari Rais William Ruto ameelekea China kwa sababu hiyo.
Inaaminika kwamba mkutano huo ambao utawaleta pamoja viongozi wa mataifa ya Afrika ni jukwaa bora la Odinga kujipigia debe katika azma yake ya kumrithi Moussa Faki Mahamat katika umoja wa Afrika – AU.
Kulingana na mmoja wa wenyeviti wa kundi la kampeni ya Odinga ya wadhifa wa mwenyekiti wa tume ya umoja wa Arika AUC Elkanah Odembo ni muhimu kwa Raila kutumia fursa ya kongamano hilo.
Kenya inatarajia kupokea mkopo wa shilingi bilioni 40 kutoka kwa China za kusaidia kukamilisha miradi iliyokwama ya maendeleo humu nchini.