Raila atua Msumbiji kutafuta uungwaji mkono wa uenyekiti wa AUC

Martin Mwanje
1 Min Read
Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga akiwa na Rais wa Msumbiji Daniel Francisco Chapo

Azima ya Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga kutaka kuwa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC imempeleka nchini Msumbiji kutafuta uungwaji mkono wiki chache kabla ya uchaguzi wa wadhifa huo kufanyika mwezi ujao. 

Akiwa nchini Msumbiji, Raila amekutana na Rais mpya wa nchi hiyo Daniel Francisco Chapo na kumwelezea maono yake ya bara la Afrika.

Raila amekuwa akizuru mataifa mbalimbali ya bara hilo na kukutana na viongozi wake ili kuwashawishi kumuunga mkono wakati wa uchaguzi huo.

Miongoni mwa mataifa ambayo ametembelea kufikia sasa ni Chad, Mauritius, Togo, Afrika Kusini, Zimbabwe na Morocco.

Wadhifa wa mwenyekiti wa AUC kwa sasa unashikiliwa na Moussa Faki kutoka Chad.

Itamlazimu Raila kuwatema Waziri wa Mambo ya Nje wa Djibouti Mahamoud Ali Youssouf na Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Madagascar Richard Randriamandrato ambao pia wanamezea mate wadhifa huo kabla ya kuibuka mshindi.

Raila anasema kukabiliwa na upinzani mkali hasa kutoka kwa Youssouf.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *