Raila apendekeza kaunti kuongezewa mgao wa pesa hadi asilimia 35

Dismas Otuke
0 Min Read

Kiongozi wa muungano wa upinzani Raila Odinga amependekeza mgao wa pesa kwa kaunti kuongezwa kutoka asilimia 15 hadi 35.

Raila amesema pendekezo hilo litakuwa katika maoni yao kwa mazungumzo kati ya serikali na upinzani yanaoendelea katika ukumbi wa Bomas of Kenya.

Kiongozi huyo ameitaka pia serikali kukoma kuhitilafiana na utendakazi wa kaunti na mfumo wa ugatuzi.

Website |  + posts
Share This Article