Raila aingilia kati kupunguza joto la kisiasa ODM

Martin Mwanje
1 Min Read

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga amewataka viongozi wanaopigania uongozi wa chama hicho kutuliza uhasama unaoweza kukisambaratisha. 

Mirengo kadhaa ya kisiasa imeibuka chamani humo tangu Raila atangaze kuwa atawania wadhifa wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC.

Kunao viongozi wanaomuunga mkono Gavana wa zamani wa kaunti ya Mombasa Hassan Joho kuwa kiongozi mpya wa ODM huku wengine wakimshabikia Gavana wa zamani wa kaunti ya Kakamega Wycliffe Oparanya.

Kwa upande mwingine, mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino ameapa kufanya kila awezalo kuhakikisha anatwaa uongozi wa ODM endapo Raila atachaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa AUC.

“ODM ni chama cha kitaifa. Hatutaki kampeni hizi zinazoweza kukigawanya chama kwa misingi ya kimaeneo,” alisema Raila wakati kampeni za kurithi wadhifa wake ODM zikichacha.

“Ni vizuri kwamba baadhi ya watu wametoa maoni yao kwamba wanamtaka Hassan Joho lakini hawasemi hivyo kwa sababu anatokea Pwani. Wacha wengine waseme Oparanya na wengine Raila. Wakati ukiwadia tutaamua kama chama.”

Share This Article