Raia watatu wa Israel wauawa na wapiganaji wa Palestina

Tom Mathinji
1 Min Read

Raia watatu wa Israel wameuawa na wengine 16 kujeruhiwa, baada ya wapalestina wawili waliokuwa wamejihami kwa bunduki kufyetua risasi katika kituo kimoja cha mabasi kilichokuwa kimejaa watu magharibi mwa Jerusalem, haya ni kwa mujibu wa polisi wa Israeli.

Video ziliwaonyeasha washambulizi hao wakitoka kwenye gari katika barabara moja kuu na kuwashambulia watu kwa risasi.

Maafisa wa usalama ambao hawakuwa kazini na raia mmoja waliokuwa mahala pa shambulizi hilo, waliwaua washambulzi hao ambao polisi wamesema walitoka Jerusalem mashariki.

Kundi la Hamas limedai washambulizi hao ni wanachama wake huku likisema shambulizi hilo lililikuwa la kulipiza kisasi uhalifu unaotekelezwa na Israeli katika ukanda wa Gaza na kwingineko.

Aidha shambulizi hilo lilitekelezwa saa chache baada ya Hamas na Israeli kukubaliana kuendelea kusitisha makabiliano kwa siku zingine saba ili kuwezesha kuendelea kuachiliwa kwa mateka wa Israeli na wafungwa wa Palestina.

TAGGED:
Share This Article