Raia wa Sierra Leone washiriki uchaguzi mkuu

Tom Mathinji
1 Min Read

Raia wa Sierra Leone wanapiga kura kwenye uchaguzi mkuu baada ya kampeni zilizokumbwa na ghasia.

Siku ya Jumatano, chama kikuu cha upinzani kilidai kuwa mfuasi wao aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi lakini polisi wamepinga madai hayo.

Wafuasi wa vyama viwili vikuu wameshtumiwa kwa kuwashambulia wapinzani.

Uchaguzi huo unajiri huku uchumi wa nchi hiyo ukidorora, gharama ya maisha kupanda na wasiwasi kuhusiana na uwiano wa taifa hilo.

Wapiga kura wanamchagua Rais, wabunge na madiwani kwenye uchaguzi wa tano katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipomalizika mwaka 2002.

Mzozo huo uliodumu kwa miaka 11 ulisababisha vifo vya takriban watu 50,000.

Rais Julius Maada Bio, mwenye umri wa miaka 59 wa chama cha Sierra Leone People’s Party, anawania kipindi cha pili cha miaka tano.

Mpinzani wake mkuu miongoni mwa wagombea 12, ni Dakta Samura Kamara mwenye umri wa miaka 72 wa chama cha All People’s Congress.

TAGGED:
Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *