Rachel Ruto kufanya mazungumzo na Malkia Camilla

Tom Mathinji
1 Min Read
Mama Taifa rachel Ruto

Mama taifa Rachel Ruto atafanya mazungumzo na Malkia Camilla wa Uingereza ambaye ameandamana na mume wake Mfalme Charles wa tatu katika ziara rasmi ya siku nne hapa nchini.

Kupitia kwa taarifa, afisi ya mama taifa ilisema miongoni mwa mazungumzo kati ya viongozi hao wawili ni kuhusu miradi ya kuwawezesha wanawake kiuchumi.

Ziara hiyo ya kifalme ni ya kwanza katika taifa la Afrika tangu walipotawazwa  mwezi Mei mwaka huu.

Mfalme Charles wa tatu na Malkia Camilla waliwasili hapa nchini Jumatatu saa tano usiku, wakitumia ndege ya jeshi la wanahewa ya Uingereza.

Walipowasili hapa nchini, walikaribishwa na waziri mwenye mamlaka makuu ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje Musalia Mudavadi.

Website |  + posts
Share This Article