Qatar Airways yasitisha safari zake baada ya anga kufungwa

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirika la Ndege la Qatar Airways limetangaza kusitisha safari zake za Ndege kwa muda kutokana na kufungwa kwa anga.

Uamuzi huo umechukuliwa kwa kuzingatia hali ya usalama wa usafiri wa anga, huku Shirika hilo likisema usalama wa abiria na Wafanyakazi ni kipaumbele cha kwanza.

Kufungwa huko kwa anga kumejiri baada ya Marekani na Israel kuanzisha mashambulizi ya angani dhidi ya Iran, huku Rais Donald Trump akisema Operesheni kubwa za Kivita zinaendelea.

Share This Article