Rais wa Urusi Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wanakutana Vostochny Cosmodrome.
Viongozi hao wawili walisalimiana, shirika la habari la Urusi TASS linaripoti.
“Nimefurahi kukuona,” Putin alimwambia Kim alipokuwa akimkaribisha kiongozi wa Korea Kaskazini kwenye kituo cha anga ya juu ya Urusi.
“Huu ni uwanja wetu mpya wa ulimwengu,” Putin aliongeza, akimtambulisha kwa kituo cha anga cha Vostochny kilichozinduliwa mnamo 2016.
Kisha Kim alimshukuru Putin kwa mwaliko huo, kwa mujibu wa video iliyochapishwa kwenye kituo cha Telegram cha Kremlin.
Hayo yanajiri wakati ambapo kuna uthibitisho kutoka kwa Korea Kusini kwamba Kaskazini ilirusha makombora mawili ya masafa mafupi.
Jeshi la Korea Kusini lilisema kuwa makombora hayo yalirushwa kutoka eneo la Sunan huko Pyongyang hadi Bahari ya Mashariki kuanzia saa 11:43 asubuhi (02:43 GMT) hadi 11:53am kwa saa za huko.
Bado hawajatambua ni aina gani ya kombora. Nchi hiyo imefanyia majaribio makombora kadhaa ya balistiki na cruise katika miaka ya hivi karibuni, licha ya Umoja wa Mataifa kupiga marufuku programu yake.