Prof. Kisiang’ani ateuliwa mshauri wa masuala ya uchumi wa Rais

Martin Mwanje
1 Min Read
Prof. Edward Kisiang'ani - Katibu wa Habari, Mawasiliano na Uchumi Dijitali

Katibu katika Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Dijitali Prof. Edward Kisiang’ani ameondolewa kwenye wadhifa huo katika mabadiliko ya hivi karibuni yaliyofanywa na Rais William Ruto serikalini. 

Tangu kubuniwa serikali ya Kenya Kwanza, Prof. Kisiang’ani amehudumu kama Katibu katika Idara ya Utangazaji na Mawasiliano katika Wizara hiyo.

Katika mabadiliko ya hivi punde, Prof. Kisiang’ani ameteuliwa kuwa Mshauri Mwandamizi na Mwanachama wa Baraza la Rais la Washauri wa Masuala ya Uchumi.

Kwa upande mwingine, Amos Gathecha amepandishwa cheo kwa kuteuliwa kuwa Naibu Mkuu wa Utumishi wa Umma katika Ofisi Kuu ya Rais.

Awali, Gathecha alihudumu kama Katibu katika Wizara ya Utumishi wa Umma.

Website |  + posts
Share This Article