Bingwa mara tatu wa dunia karika mbio za mita 1500 Faith Kipyegon alinyakua taji ya Diamond League kwa mara ya tano, baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo katika mkondo wa 14 na wa mwisho ulioandaliwa mjini Eugene nchini Marekani maarufu kama Prefontaine Classic Jumamosi usiku.
Kipyegon ambaye pia ni bingwa mara mbili wa Olimpiki aliibuka mshindi kwa dakika 3 sekunde 50 nukta 72.
Simon Koech alinyakua ushindi katika mita 3,000 kuruka viunzi na maji kwa mara ya kwanza akitumia dakika 8 sekunde 6 nukta 26.
Ferdinand Omanyala alifunga msimu wa mita 100 alipomaliza nafasi ya tatu kwa sekunde 9 nukta 85 nyuma ya Wamarekani Christian Coleman na Noah Lyles walichukua nafasi za pili kwa sekunde 9 nikta 83 na sekunde 9 nukta 85 mtawalia.
Beatrice Chepkoech alimaliza wa pili katika mita 3000 kuruka viunzi na maji nyuma ya Wilfred Yavi Mutile wa Bahrain huku Faith Cherotich akichukua nafasi ya tatu.