Posta wadinda kupigwa dafrau na wenyeji Homeboyz ligi kuu FKF

Dismas Otuke
1 Min Read

Posta Rangers wamelazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Kakamega Homeboyz,katika mchuano wa pekee wa ligi kuu wa kati  kati ya wiki, uliosakatwa Alhamisi jioni katika uwanja wa Bukhungu.

Moses Shumah aliwaweka kifua mbele wenyeji kunako dakika ya saba, lakini viongozi wa ligi Posta wakarejea mchezoni kwa goli la dakika ya 30 la kiungo Benard Ondiek.

Rangers wanaongoza jedwali kwa alama 20,moja zaidi ya mabingwa watetezi Gor Mahia baada ya mechi 9 za msimu.

 

Website |  + posts
Share This Article