Polisi wamewafurusha wanafunzi wa shule ya wasichana ya Butere kutoka kwa tamasha la muziki, sanaa na maigizo awamu ya kitaifa linaloendelea katika ukumbi wa Melvin Jones, kaunti ya Nakuru.
Wanafunzi hao wameagizwa kuondoka ukumbini kutokana na mchezo wao wa kuigiza waliopanga kuwasilisha kwa kichwa “Echoes of War” kwa madai ya kuchochea uhasama.
Wanahabari na raia pia wamezuiwa kuingia ukumbini kutazama tamasha hilo huku pia polisi wakifyatua vitoza machozi kuwatawanya wananchi waliotaka kuzua rabsha baada ya wanafunzi hao kufurushwa.
Mwenyekiti wa chama cha KANU, Gideon Moi, amekashifu serikali kwa kuwanyima wanafunzi hao fursa ya kutumia kipaji chao.