Polisi wathibitisha kufariki kwa watu 49 kutokana na mafuriko

Mvua kubwa ilinyesha Machi 6 na kusababisha mafuriko yaliyoathiri hasa jiji la Nairobi. Watu zaidi ya 2,000 wamepoteza makazi.

Martin Mwanje
1 Min Read

Idadi ya watu waliofariki kote nchini kutokana na mafuriko yaliyoshuhudiwa Ijumaa wiki iliyopita imefikia 49. 

Familia zaidi ya 2,000 pia zimeripotiwa kupoteza makazi.

Huduma ya Taifa ya Polisi, NPS, inasema inashirikiana na asasi zingine kuendeleza shughuli za uokozi na utafutaji, uhamishaji wa wakazi katika maeneo hatari na utoaji wa usalama.

“Kufuatia mvua kubwa iliyoshea Ijumaa, Machi 6, 2026, watu 49 kwa bahati mbaya wampoteza maisha kote nchini kutokana na mafuriko,” ilisema NPS kupitia msemaji wake Muchiri Nyaga kwenye taarifa.

“Jumla ya familia 2, 624 zimepoteza makazi yao. Miundombinu na mali pia zimeharibiwa katika maeneo mbalimbali nchini, vikiwemo vituo 16 vya polisi ambavyo vimeathiriwa.”

NPS inasema inafanya kazi usiku na mchana kuzipiku changamoto zilizosababishwa na mafuriko hayo.

Huduma hiyo inatoa wito kwa raia kuendelea kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa za hivi punde zinazotolewa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa na asasi zingine husika za serikali.

 

Share This Article