Polisi wataka ushirikiano wa wafanyabiashara Nairobi ili kuimarisha usalama

Tom Mathinji
2 Min Read

Huduma ya Polisi nchini Kenya imewataka wafanyibiashara kushiriana na vyombo vya dola katika harakati za kuimairisha usalama katika maeneo ya kufanyia bioashara.

Kamanda wa polisi kaunti ya Nairobi Adamson Bungei, alikariri kujitolea kwa maafisa wa usalama kuitikia kwa haraka mwito wa mashirika wakati wa dharura za kiusalama hali ambayo iemchangia mazingira bora yta kufanya biashara.

Polisi wakihudhuria ibada ya maombi

Bungei aliwataka wamiliki wa mikahawa kushirikiana na polisi katika uimarishaji usalama katika juhudi za kutangaza Nairobi kama kituo bora cha utalii ulimwenguni.

“Tunatumia mfumo wa uhitaji katika harakati zetu za kukabiliana na utovu wa usalama katika kaunti ya Nairobi.Kuwashirikisha wananchi kunatusaidia kubuni mbinu mwafaka za kutatua ukosefu wa usalama na kubuni mazingira bora kufanyia biashara.”akasema Bungei

Jackton Amutala, ambaye ni mkurugenzi wa utendakazi na ustawi wa biashara katika mikahwa ya PrideInn, akikariri mchango mhimu wa sekta hiyo katika uchumi wa nchini na kuahidi kushirikiana na vyombo vya usalama kuhakikisha usalama wa wateja wao katika kaunti ya Nairobi.

“Kuimarika kwa usbhirikiano kati ya sekta ya mihakama na utalii na vyonbo vya usalama imeimarisha usalama katika mikahawa ya kaunti ya nairobu na hivyo kusababisha ongezeko la watalii wa ndani na wale wa nje.”akasema Amutala

Wawili hao walisema haya ijuamaa walipohudhuria ibada ya maombi kwa idara ya polisi katika chuo cha mafunzo ya polisi eneo la South C, ambapo mkahawa wa Pride Inn uliandaa staftahi kwa zaidi ya maafisa 200 .

Website |  + posts
Share This Article