Polisi wapata mifugo 70 walioibwa Isiolo

Dismas Otuke
0 Min Read

Maafisa wa polisi kutoka kaunti ndogo ya Isiolo wamepata na kuwarejesha mifugo 70 walioibwa.

Yamkini polisi walikabiliana vikali na wezi wa mifugo katika milima ya Lowangishu, kabla ya wezi hao kuzidiwa na kutoroka huku wakiwaacha nyuma mifugo.

Mifugo hao walioripotiwa kuibwa kutoka kwa walishaji kutoka eneo la Matambithi, kaunti ya Meru, tayari wamerejeshewa wamiliki halisi.

Share This Article