Polisi wanasa kilo 1,500 za nyama ya punda, Embu

Washukiwa watatu wakiwemo dereva wamekamatwa huku uchunguzi ukianzishwa kuhusu chanzo cha biashara hiyo haramu na kuwakamata wahusika wote.

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa polisi wamenasa kilo 1,500 za nyama ya punda mjini Embu, iliyokuwa ikisafirishwa kuelekea mahali kukisojulikana na kuwaonya wananchi dhidi ya kununua nyama wanayoishuku.

Maafisa kutoka kitengo cha uchunguzi wa kesi za jinai DCI waliokuwa wamearfiwa kuhusu uovu huo, walilisimamisha gari hilo aina ya Probox kwenye barabara kuu ya Kiritiri-Embu mapema asubuhi.

Baada ya kukagua gari hilo, polisi walipata nyama ya punda iliyopakiwa ndani ya magunia 15 yaliyopakiwa kando pamoja na gunia jingine lililokuwa limepakiwa sehemu uzazi za wanyama hao linalokisiwa kupelekwa katika soko maalum.

Washukiwa watatu wakiwemo dereva wamekamatwa huku uchunguzi ukianzishwa kuhusu chanzo cha biashara hiyo haramu na kuwakamata wahusika wote.

Kisa hicho kinajiri miezi mitatau tu baada ya polisi kunasa mizoga ya punda 20 waliochinjwa katika boma moja eneo bunge la Runyenjes, Disemba 22 na kuzua hofu kuhusu ongezeko la uchinjaji na uuzaji wa haramu wa nyama ya punda katika kaunti ya Enbu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *