Polisi mjini Ol kalou katika kaunti ya Nyandarua wamenasa bhangi ya thamani ya takribani shilingi milioni 4,ikiwa kwenye gari la kibinafsi.
Akithibitisha kisa hicho,Kamanda wa polisi katika kaunti ya Nyandarua Omar Arero amesema kwamba gari hiyo aina ya Toyota Wish inaaminika kutoka kaunti ya Migori na ilikuwa ikielekea Nairobi.
Gari hiyo ilinaswa katika barabara kuu ya kutoka Nakuru kuelekea Ndundori kuelekea Ol,kalou katika kaunti ya Nyandarua.
Arero amesema mtu mmoja ametiwa ambaye ni dereva wa gari hiyo alikamatwa na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Ol, Kalou akisubiri kufikishwa mahakamani wakati wowote.
Aidha mkuu huyu wa polisi katika kaunti ya Nyandarua Omar Arero amesema kwamba gari hiyo ina nambari mbili tofauti za usajili kinyume cha sheria.
Amewataka wananchi kushirikiana na idara ya usalama katika kaunti ili kukomesha biashara na matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo pombe haramu ambayo kwa sasa imekita mizizi.