Polisi wanamsaka mshukiwa mkuu wa mauaji ya Seth Nyakio Njeri

Tom Mathinji
1 Min Read
Ken Kimathi Gichunuku mshukiwa wa mauaji.

Maafisa wa polisi wanamtafuta Ken Kimathi Gichunuku, almaarufu  “Sultan,” ambaye anadaiwa kuwa mshukiwa mkuu katika mauaji ya Seth Nyakio Njeri, ambaye mwili wake ulipatikana katika nyumba ya rafiki yake mtaani Biafra, Thika, mnamo Oktoba 10, 2024.

Kulingana na idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (DCI), Gichunuku alitoroka eneo la mkasa baada kutekeleza mauaji hayo.

Kupitia mtandao wa X, DCI imesema mshukiwa huyo ana historia ya uhalifu, ambapo Septemba 25,2024, alikabiliwa na kesi dhidi ya utoaji vitisho, huku polisi wakimtaja kuwa hatari kwa yeyote atakayemfichua.

Idara hiyo imetoa wito kwa yeyote aliye na habari kuhusu aliko mshukiwa huyo, kuwasiliana na kituo cha polisi kilicho karibu.

TAGGED:
Share This Article