Maafisa wa polisi wanachunguza mauaji ya mwanamke yaliyotekelezwa na watu wasiojulikana katika mtaa wa Embakasi, Jijini Nairobi.
Kulingana na idara ya upelelezi wa makosa ya jinai DCI, mwanamke huyo anadaiwa alinyongwa na watu wawili katika mtaa wa Jua Kali, Embakasi.
DCI ilisema mauaji hayo yalitokea usiku wa kuamkia Jumanne, na yaliripotiwa na wakazi wa Eno hilo.
Idara hiyo ilisema, wakazi hao walisikia mvutano nyumbani kwa mwathiriwa mwendo wa saa sita usiku na walipofina waliwaona watu wawili wakitoroka.
Maafisa wa polisi walipofika katika eneo la mkasa, walipata mwili wa mwanamke huyo anyeaminika kuwa wa umri wa miaka 20 mambo ulikuwa na alama za kunyongwa.
Mwili huo imepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti, kusubiri upasuaji.