Polisi wamwagwa jijini Nairobi kuzuia maandamano ya Gen Z

Dismas Otuke
1 Min Read

Idadi kubwa ya polisi wa kupambana na ghasia wanashika doria katikati ya jiji la Nairobi kuzuia maandamano ya vijana wa Gen Z siku yaliyopangwa kufanyika leo Alhamisi.

Maandamano hayo yanalenga kuishurutisha serikali kufanya mabadiliko na kutimiza ahadi ilizotoa kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Halaiki ya polisi wametumwa kufuatia agizo la kaimu Inspekta Mkuu wa Polisi Douglas Kanja ambaye jana Jumatano, alitangaza kupiga marufuku maandamano yoyote katikati ya jiji la Nairobi leo Alhamisi.

Maafisa wengine wamepiga kambi katika eneo la Uhuru Park, ambapo ilidaiwa vijana hao walipanga kukutana leo.

Maandamano hayo pia yamepangwa kufanyika kote nchini.

Watu 50 wamefariki tangu kuanza kwa maandamano hayo ya vijana mwezi uliopita.

Mamia ya wengine wanauguza majeraha yanayodaiwa kusababishwa na maafisa wa polisi ambao kwa sasa wanachunguzwa na Mamlaka Huru ya Kusimamia Utendakazi wa Polisi, IPOA.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *