Maafisa wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI), wamemkamata mshukiwa mwingine kwenye mauaji ya meneja wa maswala ya wafanyakazi wa kampuni ya Wells Fargo Willis Ayieko.
Duncan Onyango, almaarufu Otuch, alikamatwa katika maficho yake katika kaunti ndogo ya Bondo.
Mshukiwa aliyekuwa amekamatwa awali, alitambua nyumba ya Duncan Onyango, kuwa mahala ambapo mwathiriwa aliteswa na kisha kuuawa.
Mwili wa mwathiriwa ulipatikana mita 400 kutoka nyumba ya mshukiwa huyo iliyo katika eneo la Luanda kaunti ya Kakamega.
Willis Ayieko aliripotiwa kutoweka Oktoba 18, 2024, baada ya kuhudhuria mazishi huko Gem.
Mwili wake ulipatikana Oktoba 23, 2024, katika eneo la Mungoware kwenye mpaka kati ya Siaya na Kakamega.