Polisi wamkamata mshukiwa anayedaiwa kutuma jumbe za vitisho mtandaoni

Tom Mathinji
1 Min Read
Shedrack Omondi Okindo akamatwa kwa kueneza jumbe za vitisho mitandaoni.

Maafisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), wamemkamata mshukiwa anayedaiwa kutuma jumbe za vitisho vya ghasia kwenye mitandao ya kijamii.

Shedrack Omondi Okindo, almaarufu Hon. Mosquito, amehusishwa na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya TikTok mnamo Agosti 1, 2025, iliyokuwa na jumbe za uchochezi na vitisho.

Kufuatia uchunguzi wa kisayansi, maafisa wa usalama walimfuata na kumpata kweye maficho yake eneo la Miritini kaunti ya Mombasa na kumkamata.

Baada ya kufanya upekuzi katika nyumba yake, maafisa hao walipata mavazi yanayotumiwa na maafisa wa usalama, kijitabu kilichokuwa na maandishi yaliyosema ” Tutatumia mbinu ya guerilla kuhakikisha haki kwa mashujaa wa uhuru,” simu tatu za mkononi, stakabadhi kadhaa zinazohusiana na chama cha  Justice Direction miongoni na vitu vingine.

Okindo kwa sasa anazuiliwa na polisi, akitarajiwa kufikishwa mahakamani.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article