Polisi wamkamata mshukiwa anayedaiwa kupanga ghasia Embu

Tom Mathinji
1 Min Read
Mshukiwa anayedaiwa kupanga ghasia Embu, akamatawa na polisi.

Maafisa wa polisi wamemkamata mshukiwa anayedaiwa kupanga ghasia zilizoshuhudiwa katika siku za hivi majuzi kaunti ya Embu.

Baada ya kutekelezwa kwa operesheni kali, maafisa wa kitengo cha Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), walimkamata Joseph Mbira Thuku ambaye anashukiwa kupanga ghasia zilizoshuhudiwa Embu.

Kupitia ukurasa wa X, idara ya DCI ilisema mshukiwa huyo alifikishwa kwenye mahakama ya Kahawa kufunguliwa mashtaka.

“Thuku, ambaye ametambuliwa kama mmoja wa waliopanga maandamano ya ghasia, alikamatwa na kufikishwa katika mahakama ya Kahawa,” ilisema DCI kwenye taarifa yake.

Mahakama hiyo iliwaruhusu maafisa hao wa polisi kumzuilia mshukiwa huyo kwa siku tano, kuwapa fursa kukamilisha uchunguzi.

Kesi hiyo itatajwa Agosti 4, 2025.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article