Huduma ya taifa ya Polisi imeharamisha maandamano yaliyokuwa yamepengwa kuandaliwa leo katika maeneo kadhaa nchini, ikisema kuwa wapangaji wa maandamano hawakufahamisha polisi wala kupata kibali.
Taarifa hiyo imesema kuwa waliopanga maandamano wamekiuka utaratibu wa kisheria uliowekwa kisheria hivyo basi maandamano hayo ya amani yaliyopangwa ni kinyume cha sheria za nchi.
Habari zimezagaa katika mitandao ya kijamii kuhusu maandamano hayo yaliyopangwa na vijana kutoa malalamishi yao kwa serikali.
Polisi wamewataka wananchi kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kuonya kukabiliana na waandamanaji wowote watakaotatiza amani au kusababisha usumbufu.