Polisi wachunguza kifo cha afisa wa idara ya uvuvi Kwale

Marion Bosire
1 Min Read

Maafisa wa polisi wanaendeleza uchunguzi kuhusu kifo cha Martin Kiogora ambaye amekuwa akihudumu kama mkurugenzi wa idara ya masuala ya kilimo, uvuvi na ufugaji katika kaunti ya Kwale.

Jumapili Agosti 20, 2023 asubuhi mwili wa Kiogora ulipatikana kitandani kwenye nyumba yake ya kupangisha mjini Kwale kaunti ndogo ya Matuga.

Mmiliki wa nyumba kwa jina Francis Kanguno alikwazwa na hatua ya Kiogora ya kuacha mlango wake wazi kuanzia Jumamosi jioni, kinyume na kawaida yake, ndiposa akalazimika kwenda kujua ni kwa nini.

Alipata mpangaji wake akiwa amefariki na mara moja akawajulisha maafisa wa polisi.

OCPD wa eneo la Kwale William Cheruiyot alithibitisha kifo cha Kiogora akisema mwili wake haukuwa na majeraha yoyote na hivyo wameanzisha uchunguzi kufahamu kilichosababisha kifo chake.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *