Polisi wa Ufaransa waondoa wahamiaji jijini Paris siku 100 kabla ya michezo ya Olimpiki

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa polisi nchini Ufaransa wamewaondoa mamia ya wahamiaji wa asili ya kiafrika kutoka katiati ya jiji la Paris, siku 100 kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki.

Polisi walitekeleza msako huo Jumatanno alfajiri wakati akina mama na watoto waliojifunika kwa mahema ,blanketi na karatasi za plastiki ili kujikinga kutokana na mvua, na kuwaamuru kubeba virago vyao na kuabiri basi hadi mji wa Besancon ulio mashariki ya Ufarana.

Wengi wa wahamiaji hao ni wa mataifa ya Afrika yanayozungumza Kifaransa kama vile Burkina Faso, Guinea, Ivory Coast na Senegal.

Makundi ya kijamii pia yametoa mchango wa mablanketi na vyakula ili kuwasaidia wahamiaji hao.

Mji wa Paris utaandaa makala ya 33 ya michezo ya Olimpiki kati ya Julai 26 na Agosti 11, huku wanamichezo wapatao 10,500 wakitarajiwa kushindana katika michezo 329 ya fani 32.

Share This Article