Polisi wa Kenya waimarisha doria mjini Port-au-Prince kufuatia kuawa kwa watu 200

Dismas Otuke
1 Min Read

Polisi wa Kenya wakishirikiana na wengine kutoka ujumbe wa usalama wa Umoja wa Mataifa, UN waliimarisha usalama katika jiji kuu la Haiti, Paort-Au- Prince, kufuatia mauji ya raia 200 mwishoni mwa juma lililopita.

Polisi hao wamekiri kutwaa kituo cha pili cha polisi kilichokuwa kimetwaliwa na magenge ya majambazi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mauaji ya mwishoni mwa juma lililopita yalifikisha idadi ya raia waliouawa na magenge ya wahalifu kuwa zaidi ya 5,000, tangu mwanzo wa mwaka huu nchini Haiti.

Magenge hayo yanadhibiti zaidi ya asilimia 80 ya mji wa Paort-Au- Prince huku watu takriban laki saba wakifurushwa makwao, kwa mujibu wa takwimu za UN.

Kenya ina jumla ya polisi 400 waliotumwa kwa opereshi hiyo ya kushika doria nchini Haiti tangu mwezi Juni mwaka huu.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *