Polisi wa Kenya kushika doria Haiti kwa mwaka mmoja zaidi

Dismas Otuke
1 Min Read

Polisi wa Kenya wanaohudumu nchini Haiti wataendelea kuhudumu kwa miezi 12 zaidi, baada ya baraza la Umoja wa mataifa kuidhinisha kuongeza muda wake.

Kenya ina polisi wapatao 400 kati ya jumla ya maafisa wa usalama 2,500 wanaoshika doria nchini Haiti, ili kurejesha utulivu kufuatia magenge ya majangili ambao walikuwa wametwaa maeneo mengi katika mji mkuu wa Port Au Prince  na kusababisha raia wengi kutoroka makwao.

Vikosi hivyo vy usalama vilivyo Haiti vinajumuisha vya kutoka Belize,Benin,Bahamas,Bangladesh,Barbados,Jamaica na Chad.

Umoja wa mataifa unatarajia kuongeza ufadhili kwa opareshini hiyo wakati pia Kenya ikipanga kutuma polisi 600 zaidi kutimiza idadi ya maafisa 1,000, ambao Rais William Ruto waliafikiana na Marekani kutuma kisiwani humo.

Haya yanajiri takriban wiki moja baada ya Rais Ruto kufanya ziara ya ghafla nchini Haiti kukagua maendeleo ya polisi wa Kenya.

Share This Article