Police FC yawatema wakufunzi wote kwa msururu wa matokeo mabovu

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Police FC imewapiga kalamu wakufunzi wote kufuatia msururu wa matokeo mabovu ya timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu ambapo inashikilia nafasi ya 15 kwa pointi 6.

Kocha wa timu ya wanawake Beldine Odemba amekabidhiwa mikoba japo kwa muda, hadi pale mkufunzi wa kudumu atakapoteuliwa.

Timu hiyo ya maafande imekuwa chini ya uongozi wa kocha Salim Babu, aliyeiongoza kumaliza ya tatu ligini msimu jana kwa alama 57.

Masaibu ya Police FC yalianza baada ya kumteau Anthony Kimani kuwa kocha mkuu akisaidiwa na Babu kwani alikuwa na leseni ya CAF A, ili kuafiki viwango vya shirikisho la soka barani Afrika CAF.

Police FC waliendeleza matokeo duni msimu huu licha kuwasajili wanandinga Jesse Were, Daniel Sakari, Jackson Macharia, Alfred Leku na Brian Musa mwanzoni mwa msimu huku wakitimuliwa na Zamalek FC katika mchujo wa kwanza wa kombe la shirikisho.

Website |  + posts
Share This Article