Police Bullets FC yapata leseni ya CAF

Dismas Otuke
2 Min Read

Klabu ya Police Bullets FC, imepata Leseni maalum ya CAF, kutoka kwa bodi ya FKF, ambayo inawatambua kama wawakilishi rasmi wa Kenya katika mashindano ya kombe la Shirikisho ya Vilabu kwa soka la wanawake, 2025/26 CAF Women’s Champions League.

Police Bullets, ilipata fursa ya kuwakilisha kenya katika mashindano haya makubwa kwa ngazi ya vilabu, baada ya kufanyiwa tathmini kwa mujibu wa vigezo vitano vilivyowekwa na shirikisho la soka Afrika, CAF.

Nguzo hizo ni pamoja na Michezo, Sheria na Fedha, Miundombinu,Utawala na Rasilimali Watu.

Tathmini hiyo, iliyoendeshwa na Shirikisho la Soka Afrika CAF, kupitia Jukwaa la Mtandaoni la Leseni kwa Vilabu (CLOP).

Vigezo hivyo, vinavihitaji vilabu kuwasilisha nyaraka za kina za vipengele 34, kabla ya kuruhusiwa kushiriki michuano yoyote ya Ligi ya mabingwa ya soka la wanawake au kombe la shbirikisho.

Rais wa Shirikisho la soka nchini (FKF), Hussein Mohamed ameonesha kuridhishwa na taarifa hizo, kwa mujibu wa taarifa yake. Katika taarifa hiyo, Husein alisema: “Zoezi hili limethibitisha kuwa kama taifa, tuko tayari kwa ajili ya maendeleo ya soka.”

“Police Bullets FC, ni ithibati tosha ya jinsi tunavyoweza kupiga hatua kisoka, hasa tunapoamua kuwekeza juhudi na mali, katika kukuza soka la wanawake. Bullets ndio klabu pekee nchini ambapo, kila mchezaji ana mkataba wa kisheria na klabu.”

Share This Article