Mabingwa watetezi Kenya Pipeline watazundua uhasama na APR kutoka Rwanda kwenye fainali ya taji ya Africa Zone V mjini Kampala Uganda.
Vidosho wa Pipeline walifuzu kwa fainali baada ya kuwazaba wenyeji Sports-S seti tatu kwa bila katika nusu fainali jana.
KPC walisajili ushindi wa 25-19, 25-22, na 25-15 wakijivunia kutoshindwa mechi hata moja tangu kuanza kwa mashindano hayo.
APR nao walitinga fainali kufuatia ushindi wa seti zizo hizo 3-0 dhidi ya Uganda alama 25-16, 25-11, na 25-10.