Timu ya taifa ya Nigeria imepata pigo baada ya kiungo wake mkabaji Wilfred Ndidi kupata jeraha siku chache kabla ya michuano hiyo kuanza.
Ndidi alikuwa amejumuishwa katika kikosi cha Jose Peseiro ambacho kitacheza mashindano ya kuwania ubingwa wa Afrika mwaka wa 2023, na angekuwa kiungo muhimu katika vita vya timu hiyo vya kuwania taji la nne.
Mchezaji huyo wa safu ya kati ya ulinzi ni miongoni mwa wachezaji bora barani Afrika na pia ni mmoja wa wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika kikosi cha Super Eagles, na awali aliyeshiriki michuano ya Kombe la Dunia na Kombe la Mataifa (Nations Cup).
Kwa sasa, Peseiro kupitia mtandao wa kijamii wa X wa timu ya Super Eagles, amemtaja Alhassan Yusuf kuziba nafasi ya Ndidi. Yusuf anakipiga katika klabu ya Antwerp nchini Ubelgiji.
Kikosi cha Nigeria ambacho kimetajwa na Jose Peseiro kipo Uarabuni (Abu Dhabi) katika maandalizi kabambe ya michuano hiyo itakayoanza Januari 13, 2024 nchini Ivory Coast.
SOMA ZAIDI: Matukio manne yaliozua vilio na mijadala mikali ligi ya EPL 2023