Peter Kioi atabiri kifo chake

Alikiri kuwa amekuwa akinywa pombe licha ya kuwa na matatizo ya figo na ini

Marion Bosire
1 Min Read

Mwanamitandao wa Kenya Peter Kioi ametabiri kifo chake katika hatua iliyoshangaza wengi wa wafuasi wake mitandaoni.

Kioi ambaye ni maarufu sana kwenye mtandao wa TikTok amewaacha wakenya kwenye mitandao wakiwa na mshangao baada ya kufunguka kuhusu changamoto zake za kiafya, huku akielezea ombi lake la mwisho.

Mshawishi huyo alitabiri kifo chake na kuwaomba mashabiki wake wamsaidie mama yake wakati huo utakapofika.

Utabiri wa kifo cha TikToker huyo umewaacha Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wakimtumia ujumbe wa kumtia moyo. Alikiri kuwa amekuwa akinywa pombe licha ya kuwa na matatizo ya figo na ini.

Mshawishi huyo alitumia TikTok kukiri kuwa ana matatizo ya ini na figo na kwamba magonjwa hayo yamemdhoofisha.

Aliwaomba mashabiki wake wamtembelee mama yake na kumpa pole endapo atafariki.

“Jambo jema kwangu ni kwamba nimekubali kuwa ugonjwa huu umenidhoofisha. Kwa hiyo jambo linalofuata ni msikose tukio la kuja nyumbani kumpa pole mama yangu. Nina uhakika mwaka huu hautaisha kabla sijafariki,” alisema.

Wakenya mitandaoni walijibu utabiri wa Kioi kwa kumtaka awe na mtazamo chanya zaidi na aache kuzungumzia kifo chake. Walimkumbusha kuwa ulimi una nguvu kubwa.

Share This Article